Moyo Media Co. Ltd yatoa mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa wasaidizi wa kisheria – kisiwani Pemba

Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Chake Chake Paralegal Organization na kuhudhuriwa na baadhi ya wasaidizi wa kisheria Chake Chake, Mkoani n.k

Mada kuu ni jinsi gani ya kutumia mitandao ya kijamii kwa usahihi kwa taasisi zisizo kifaida (Non-Profit Organization pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya matumizi ya mitandao ya kijamii akifanya mazoezi kwa vitendo baada ya mafunzo
Mmoja wa wataalam kutoka Wizara ya Afya – Zanzibar akiwasilisha mada juu ya kirusi cha Korona
Mmoja wa wataalam kutoka Wizara ya Afya – Zanzibar akiwasilisha mada juu ya kirusi cha Korona

Pamoja na mafunzo hayo, pia washiriki walipata fursa za kupatiwa mafunzo kuhusu maradhi ya korona (COVID-19). Mafunzo hayo yalijikita kwa kina kuhusu korona, njia sababishi za kusambaa kwa maradhi na jinsi gani unaweza kujikinga na maradhi hayo. Mafunzo hayo yaliyohusu Korona yalitolewa na wataalumu wa afya kutoka Wizara ya Afya – Zanzibar