Moyo Media Co. Ltd yatoa mafunzo ya Usalama Mtandao kwa wadau wa Tehama kisiwani Pemba

Afisa Mtendaji Mkuu wa Moyo Media Co. Ltd ambae pia ni Raisi wa Shaibu Foundation, Nd. Mustafa Moyo akiwasilisha mada ya Usalama mtandao jana tarehe 10/11/2018 katika ukumbi wa American Corner Pemba.

Kampuni ya Moyo Media ikishirikiana na American Corner Pemba kwa kupitia harambee yake ya “LEARN & DONATE” iliyoanzishwa na kampuni hiyo pamoja na Shaibu Foundation wametoa mafunzo ya Usalama Mtandao yaani “Cyber Security” kwa taasisi mbali mbali na wadau wake kisiwani Pemba.

Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wadau kuhusiana  mabadiliko ya teknolojia, uhalifu mtandao, njia zipi wahalifu wanatumia katika kufanya uhalifu, Jinsi gani unaweza kujilinda n.k

Washiriki wakiendelea kupata mafunzo juu ya usalama mtandao.

Ingawa mashirika mengi makubwa huthamini na kuwa makini kweli juu ya hali halisi ya vitisho vyao wanakuvyotana navyo, makampuni mengi ya biashara ndogo na za kati hawafahamu au wanapuuza juu ya njia ambazo zina hatari. Kwa takribani 45% wanafikiria kuwa wao sio walengwa dhidi ya madhara ya uhalifu mtandao.

Kwa kweli, mashirika yote yanayotumia Internet yana hatari ya kushambuliwa. Na sio suala la kama utashambuliwa mpaka uwe mtu maarufu au tajiri n.k. Wengi wa mashambulizi ya cyber ni automatika yaani yanasambaa wenyewe na hayachagui, tunaweza sema ni sawa na ugonjwa ambukizi ambapo mtu yoyote anaweza ambukizwa bila kijali dini, kabila, rangi wala kipato chako, na huku ndivyo hivyo hivyo. Wahalifu hutumia udhaifu unaojulikana badala ya kulenga mashirika maalum. Shirika lako linaweza kukutwa na kadhia hiyo sasa na huenda hata usijue.

Nd. Mustafa Moyo akitoa maelezo kuhusu taasisi ya Shaibu Foundation na harambee ya LEARN & DONATE

Vile vile kwa kupitia mafunzo hayo, wadau walipata fursa ya kupewa elimu juu ya suala zima la kujitolea kkwa hiari katika kusaidia jamii bila kutegemea kupata malipo yoyote kutoka katika jamii husika au mtu.

Harambee ya CHANGIA & UJIFUNZE (LEARN & DONATE) ni endelevu ambayo inawalenga kuwajengea uwezo wanajamii hasa vijana ambao wanatafuta ajira. Ambapo watapata fursa ya kujifunza mambo mengi ili waongeze ujuzi, kwa maana nyakati hizi kuna tatizo la ukosefu wa ajira ambapo fursa ikitokea vijana wengi hukosa uzoefu katika kazi au fani husika. Kwa sababu elimu kutoka chuoni tu haitoshelezi pekee yake bali mtu analazimika pia kuwa na uzoefu wa kazi pia na baadhi ya taasisi hutumia uzoefu katika kazi kama kigezo cha uajiri ili kupunguza gharama wakati wanapomuajiri mtu.

Baadhi ya washirikia wakiwa katika picha ya pamoja

 

 

CHANZO: PEMBA LIVE

error: Content is protected !!