KUKOSEKANA KWA HUDUMA MTANDAO

REF: MM/E/2018/TO/DE30-121                                                              30-12-2018

Kwanza hatuna budi kumshukuru M/Mungu kwa kutujaalia afya njema na uhai.

Pili nitumie fursa hii kuwaomba radhi wateja wetu wote kwa usumbufu unaojitokeza ambao unatokana na kukosekana kwa huduma mtandao. Tatizo hili limeanza kujitokeza wiki mbili zilizopita, ambapo chanzo cha tatizo limetokana wakati tulipokuwa tunatekeleza zoezi la kubadilisha mifumo yetu ya kimtandao ikiwa na lengo la kuboresha usalama mtandao.

Zoezi hilo lilikamilika kwa wakati, kwa bahati mbaya baadhi ya huduma hazikurudi hewani na kupelekea baadhi ya wateja wetu kukosa huduma.

Hadi sasa, mafundi wetu wanaendelea na matengenezo ili kuhakikisha huduma zinarudi hewani kama kawaida.

Hivyo nitumie fursa hii kuwaomba radhi wateja wetu wote ambao wanaendelea kukosa huduma, tunaahidi kufanikisha zoezi hili kwa uwezo wake M/Mungu huduma zote zitarudi kwa awali zikiwa katika ubora wa hali ya juu kuliko mwanzo.

Tunawaomba tuwe wastahamilivu kwa kipindi hiki. Tunatanguliza shukrani kwa ustahamilivu wenu,

Kwa mawasiliano zaidi n.k wasiliana na timu ya ufundi kwa barua pepe ya info@moyomedia.co.tz

Ahsantum,

Mustafa Said Abdurabi,

Afisa Mtendaji Mkuu, Moyo Media Co. Ltd

error: Content is protected !!