
SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Uongozi wa kampuni ya Moyo Media pamoja na kampuni tanzu zinazomilikiwa na Moyo Media Company Limited tunatoa salamu za rambirambi kwa familia ya mjane wa Hayati, Rais Magufuli, Mama Janeth Magufuli, watoto, ndugu na jamaa kwa kuondokewa na mpendwa wao na wananchi wote wa Tanzania kwa pigo hili kubwa.
Ni msiba mzito ambao hatukutarajia, sote tunafahamu jinsi Hayati, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alivyoipenda nchi, alivyowapenda Watanzania na kujitoa kwa watu wake kwa dhamira ya dhati na nia njema ya kuibadilisha taswira ya nchi yake.
“Tumepoteza kiongozi shupavu, madhubuti, mwenye maono, mpenda maendeleo, mwana mwema wa Bara la Afrika na mwanamapinduzi wa kweli, Mhe. Magufuli alikuwa chachu ya maendeleo kwa nchi yetu na Africa kwa ujumla”
“Sisi sote ni wa Mungu na kwake tutarejea”
Imetolewa na
Afisa Mtendaji Mkuu, Kampuni ya Moyo Media